-->

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ana kilango Malecela kuanzia leo.

Anna kilango Malecela

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

 

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364