-->

Shamsa Ford Afurahia Kurudiana na Ney wa Mitego

BAADA ya kauli ya rapa Ney wa Mitego kwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford kwamba kama anachagua wasichana wa kurudiana naye atakuwa wa kwanza kutokana na ukarimu na mapenzi yake, mrembo huyo ameibuka na kufurahia kauli hiyo.

shamsaford23

Shamsa aliliambia MTANZANIA kwamba, “Mimi na Ney tuliwahi kuwa wapenzi japo tumeachana ila kiukweli tulipendana sana na kama tutarudiana hakuna tatizo kwa kuwa nampenda sana.

“Tuliachana na Ney kutokana na maneno maneno ya watu waliokuwa hawapendi penzi letu, lakini kama anataka turudiane nipo tayari,” alijieleza Shamsa huku akifurahia kauli zake hizo.

Aliongeza kuwa yeye si mnafiki kwa alichonacho moyoni na hawezi kuongea kwa kashfa kama baadhi ya waigizaji wenzake wanapotofautiana ama kuachana na waliokuwa wapenzi au waume zao.

Shamsa Ford amewahi kutamba na filamu mbali mbali ikiwepo ‘Bado natafuta’ na ‘Chausiku’.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364