-->

Rapper Chidi Benz akisamehewa na akipata msaada atarudi mahala pake!

Hakuna mtu aliyemkamilifu chini ya jua au Dunia hii tunayoishi. Chidi Benz naye ni binadamu, anamakosa yake kama mtu mwingine yeyote yule. Kwa wale aliowakosea basi hana budi kuwaomba msamaha wa dhati na najua wakijua kuna Mungu wataweza kumsamehe.

final_1

Kitendo alichofanya Meneja wa wasanii wa muziki kutoka Tip Top connection ndugu Hamisi Tale Tale maarufu kwa Babu Tale ni kitendo cha kupongezwa sana, na inabidi kila mtu kwa namna yake ya kipekee afanye la kwake analoweza kumsaidia huyu msanii wetu aliyepitiwa na kufanya makosa kama binadamu mwingine.

Kama tulivyosikia kupitia Millard Ayo TV Babu Tale amefanya lililo jema kwa upande wake la kuhakikisha anamshawishi Chidi Benz kwenda kwenye Rehabilitation Center iliyoko Bagamoyo.

Anachotakiwa kufanya Chidi Benz kwa wakati huu ni kimoja tu, nacho ni kufuata masharti yoote atakayopewa huko kwenye hiyo Centre.

Ombi kubwa hapa ni kwa wasanii wenzake na jamii kwa ujumla kumsaidia ili aweze kurudi kwenye chati kama mwanzo. Wengi wameguswa sana na Afya ya msanii huu. Wengi tunapenda sana nyimbo zake. Akiwezeshwa ninauhakika atarudi kwenye chati kama zamani na hata zaidi.

Wasanii kama Diomond, Alikiba, AY, Mwana FA, n.k. wanaweza wakamtoa Chidi Benz hapa alipo na akafika mbali. Akipata featuring na msanii yeyote hapo juu ataweza akatoka sana na pia awe anafuata ushauri kutoka kwa Meneja wake. Akipata pesa sio tena kutumbua, kuna leo na kesho afanye kweli kwa kuwekeza kwenye sehemu mbali mbali kama walivyo wasanii wengine.

Pia tunaomba nyimbo zake kwa mfano Dar es Stand up  na Mashaalah (Raga za Dunia) ni nyimbo ambazo washabiki wake wamezipenda sana. Tunaomba basi ziwekwe kwenye Ringtones (milio ya sauti za simu )  ili watu waweze kuzilipia na kuzitumia kwenye simu zao na hapo hapo kumpatia pesa ili aweze kufanya vizuri zaidi kwenye nyimbo nyingine. Ikiwezekana afanye Remix ya nyimbo hizi akiwashirikisha wasanii maarufu kama Diamond na wengine. Kuna wasanii wakishirikishwa kidogo tu, mtu anatoka. Kwanini basi wasijitolee kwa huyu kijana Chidi Benz? Fanyeni Remix kama vile mlivyofanya Zigo na ikawa bora na kupigwa kwenye TV nyingi duniani. Mungu ufurahishwa na wenye kutoa msaada kwa wenye shida na matatizo mbalimbali. Chid Benz anahitaji msaada wenu.

Pia tunaomba mitandao ya simu kama vile Tigo, nk imsaidie katika kupromote ringtones za nyimbo zake ili wateja wazilipie na kuweza kumnyanyua msanii huyu aliyekuwa ameteleza.

Nirudie tena, Babu Tale kafanya lililo jema kwa upande wake tumpongeze kwa hili na wengine tuige hili kwa kuwasaidia vijana wetu ambayo kwa namna moja au nyingine waliteleza.

Nimalizie kwa kusema, usipendezwe wala kufurahia mwenzio anapokuwa kwenye matatizo. Unatakiwa kumshukuru Mungu kwa hali uliyokuwa nayo badala ya kuanza kumcheka, kutukana au kumdhalilisha mtu.

Kama utakuwa na ushauri au maoni yeyote ktk hili basi share na wengine kwenye facebook yetu au kwenye ukurasa huu hapa chini.

Ungependa kuangalia baadhi ya video za Chidi Benz kutoka kwenye tovuti ya videozetu ?

Writer: bongomovies.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Hi there!

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364