-->

Ray: Kama Huamini Sikulazimishi, Mi Maji Yananing’arisha!

HIVI kari-buni gumzo kubwa mitaani pamoja na kwenye mitandao mingi ya kijamii ilikuwa juu ya staa wa Bongo Muvi, Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kudai kuwa kunywa maji mengi kunamfanya aendelea kuwa mweupe.

RAY987

Kauli hiyo alianza kuitoa katika mahojiano aliyofanyiwa katika Kipindi cha E-News kinachorushwa na EATV ambapo alisema kwamba huwa anakwenda saluni mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) pia na kunywa maji mengi.

“Zamani ilikuwa shida kuingia saluni kufanya scrub, sasa hivi najiweza katika hivyo vitu, kwa hiyo kwa kila wiki lazima nifanye scrub, nijitengeneze mwili wangu kama kioo cha jamii ninapotokea katika TV ili wewe Mtanzania uweze kuni-admire, kwa hiyo kimsingi sijichubui, nafanya sana mazoezi na kunywa maji mengi ndiyo siri ya ngozi yangu kunawiri,” alisema Ray.

Jamii kwa ujumla ilimchukulia tofauti na gumzo lililoenea kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na mashabiki wake wengi kufanya jaribio la kunywa maji mengi kwa mara moja huku wengine wakiunda makundi na kujiita Team Water Baby (TWB).

Showbiz Xtra ilifanikiwa kufanya mahojiano na Ray ambapo katika makala haya anafunguka yote;

Xtra: Kauli yako ya kufanya mazoezi na kunywa maji mengi, watu wengi wameichukulia tofauti, unazungumziaje hilo?

Ray: Siwezi kuwaongelea sana kwa sababu kila Mtanzania ana haki ya kuzungumza kile anachokiwaza kichwani kwake, kikubwa ninachoamini maji ndiyo yananifanya niwe na ngozi nyororo, basi! Kwa hiyo nafanya sana mazoezi na nikwambie tu hilo la kunywa maji mengi kama hawawezi basi siwezi kuwakataza ama kuwalazimisha kwangu inawezekana ndiyo maana naendelea kuwa mweupe.

Hata kwenye familia yetu hakuna mtu mweusi na kama atatokea mweusi atabakia kuwa mweusi na kama mweupe atabakia kuwa mweupe.

Xtra: Mtaani wamekuchukuliaje baada ya kuandamwa mitandaoni juu ya kauli uliyotoa?

Ray: Mtaani wanafahamu na wala hawakuona ajabu sana, wameona kama ni stori tu na kuziacha zipite.

Xtra: Lakini wapo wanaodai kuwa ulikuwa ukitafuta kiki?

Ray: Hivi kwa jinsi umri wangu huu? Nina miaka zaidi ya 15 kwenye sanaa, sasa nitawezaje kutafuta kiki? Na kwa nini isiwe kipindi kile cha nyuma na kwanza mambo hayo siyapendi kwani ninachoangalia ni kutafuta pesa na siyo kiki.

Xtra: Ratiba yako kwa siku ikoje?

Ray: Naamka saa 12 asubuhi najiandaa, saa moja asubuhi naingia gym hadi saa tatu kisha nafanya kazi za nje na baada ya hapo naendelea na mengine.

Xtra: Vipi kuhusu Nay wa Mitego unamkubali kama miongoni mwa wanamuziki wanaofanya vizuri?

Ray: Nay ni msanii kama walivyo wengine hivyo namkubali kama msanii.

Xtra: Unauzungumziaje Wimbo wa Shika Adabu Yako wa Nay wa Mitego ambao ndani yake kakuponda?

Ray: Unajua siku zote kila msanii anaamua kuimba kile ambacho ameamua kufanya kwenye kichwa chake, kwa Nay alipaswa aangalie na kile anachokiimba maana ameonesha kuwadhalilisha vibaya dada zetu lakini Basata wameshaufungia wimbo huo baada ya kuonekana hauna maadili.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364