Nilianguka Bahati Mbaya Kama Binadamu-Ray C
Ray C ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Planet bongo kinachorushwa na kituo cha EATV .
”Nilianguka bahati mbaya kama binadamu wengine ,nikajitambua sasa nipo vizuri naendelea na maisha kama kawaida japo nakumbwa na changamoto ya kutopata usaidizi kutoka kwa watu wangu wa karibu niliokuwa nao kwenye musiki zamani”Amesema Ray C
Msanii huyo amemshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kumchukulia kama mwanae na kumsaidia kupata matibabu baada ya kutumia madawa ya kulevya na kumuathiri kwa muda mrefu.
Aidha ameiomba jamii kumpokea na kumuunga mkono katika kazi zake ambazo anazifanya ambapo kwa sasa amerekodi nyimbo 5 na kuwataka waandaaji wa vipindi vya redio,televisheni na magazeti badala ya kila siku kumuandika vibaya wamuunge mkono katika jitihada zake za kurejea kwenye hali ya kawaida.
”Kuna magazeti kazi yao ni kuniandika vibaya kila siku mara nimeonekana navuta madawa kwa nini wasinipige picha kama wananiona kuliko kuandika uongo kila silku na kukatisha tamaa watu wenye lengo jema la kunisaidia”.Amesema Ray C
eatv.tv