-->

Ray Kigosi Apigilia Msumari Mwingine Kwa Batuli

 

ray677

Ray amesema kuwa, filamu hiyo itatoka kama ilivyopangwa licha ya tuhuma za Batuli, akijitetea kuwa, hawezi kushindwa kumlipa mtu mmoja na kufanikisha kuikamilisha kazi hiyo waliyoifanya miaka 3 iliyopita tayari kwa kuiingiza sokoni.

Ray pia akatolea ufafanuzi hisia zilizoanza kujengeka kuwa, wametengeneza ugomvi huo na Batuli ili kuipatia kiki kazi yao, kitu ambacho amekipinga kwa nguvu.

“ Sinema ya Tajiri Mfupi itatoka kama kawaida katika utaratibu wake jinsi ulivyopagwa, sababau hakuna msanii yoyote aliyedhulumiwa kama nimeweza kutengeneza sinema yote nikaimaliza bajeti yake ni shilingi ngapi nishidwe kulipa msanii mmoja?  Kwahiyo yeye ajaribu tu kutengeneza discipline katika kazi, kwasababu hawa dada zetu discipline katika kazi hawana kabisa, sasa hili linatakiwa liwe fundisho kwa wasanii wengine wakike kwasababu hawa wana mambo mengine wanaweza kuyafanya mabayo sisi  hatuwezi kuyafanya, nimeshaandika kwenye Instagram yangu kama amedhulumiwa kuna vyombo kama mahakama  polisi aende kushitaki au kuna chama kinaitwa TAFF cha mambo ya sinema Tanzania hapa kinatambulika kisheria, Lakini Mimi Ninahakika Kuwa Ni Movies Ambayo Ipo Sahihi Na Inatoka Kama Ilivyotakiwa Kutoka”- Ray alimaliza kueleza.

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364