Riyama Ally, My Stereo, Kuhalalisha Mahusiano Yao
Msanii wa filamu Riyama Ally, baada ya kuingia katika hatua ya Uchumba kimya kimya na mpenzi wake ambaye ni msanii chipukizi wa Bongo Fleva
leo Mysterio, amesema kuwa mpango wao wa kuhalalisha mahusiano yao umeanza kunukia, hasa baada ya msanii huyo kujihakikishia nafasi yake kwa kutoa posa.
Riyama ambaye baada ya hatua hiyo amekuwa mwepesi zaidi wa kuyazungumza mahusiano yake, hakuweka wazi tarehe rasmi ya yeye kufunga ndoa, na kuhusiana na mumewe mtarajiwa huyu hapa anaeleza mwenyewe.
Nyota huyo pia akazungumzia kubadili mtindo wake wa uigizaji, kupita filamu yake ambayo ipo njiani kutoka, ikiwa tayari imepatiwa jina la Mke Gani.
EATV.TV