-->

Roma: Nimechagua Maisha ya Shida

Nyota wa muziki wa Rap Bongo ‘Rhymes Of Magic Attraction’ Roma amethibitisha fununu za kuwa muziki anaoufanya umekua ni msalaba mzito kwenye maisha yake.

ROMA 34

Akizungumza na eNewz Roma alisema kuwa hayo ndiyo maisha aliyoyachagua na ni mwanaharakati anaetetea haki na amani katika taifa lake, maendeleo bora na hicho ndicho kitu kikubwa anachojaribu kukipigania.

“Natamani nipate utawala au uongozi ambao utamfanya Roma asiimbe hip hop na ukiona kila siku Roma anatoa mawe basi ujue bado hatujapata uongozi huo ama utawala huo,” alisema Roma na kuongeza, “Kwa hiyo inabidi niendelee kushindilia ili taifa langu siku moja lione kwamba Roma alikuwa ni mmoja kati ya wapigania haki”.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364