Rose Ndauka Kutoa Deal kwa Wasanii wa Filamu
Kampuni ya Ndauka Advert ya malkia wa filamu Rose Ndauka ikishirikiana na African Swahili TV Machi 9,10 itafanya usahili katika ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho kwajili ya kuwapata wasanii ambao watashiriki kwenye tamthilia mpya itwaayo ‘How Cheat?’.
Muigizaji huyo amewataka wasanii wakubwa kwa wadogo kuchangamkia fursa hiyo ili kujipatia ajira pamoja na kukuza vipaji vyao.
“Kipaji chako ndio mtaji wako, kipaji chako ndio ajira yako,” alisema Rose.
Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu.
Bongo5