-->

Rose Ndauka: Msiwasamehe Wanaowanyanyasa Kimapenzi

STAA wa filamu za bongo, Rose Ndauka, amewatahadharisha wanawake wenzake kwamba wasiwasamehe wanaume wanaowanyanyasa kimapenzi ndani ya nyumba zao, kwa kuwa kufanya hivyo ni kujinyima haki kisheria.

Rose alisema mwanamke anayejielewa hatakubali kunyanyasika awapo kwenye ndoa yake na anayeogopa ni yule asiyejitambua, bali anaishi ilimradi kaolewa.

“Huwa nachukizwa sana na mwanamke anayekubali kunyanyaswa katika ndoa na kujifanya mvumilivu, wakati karne hii mwanamke wa aina hiyo anadharaulika na jamii yote inayomzunguka kwa kuwa hatambui thamani yake,” alisema Rose Ndauka.

Rose aliongeza kwamba, wanawake wanaofichua manyanyaso wanayofanyiwa na wenzi wao huwa mashujaa na umma hujifunza kupitia kwao, badala ya kuficha na kuugulia ndani kwa ndani, huku ukiishia kuteketea moyoni ama kujiua.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364