-->

Samatta Aibuka Shujaa Tuzo za Afrika Huko Abuja

Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.

samatA1

Samatta mwenye umri wa miaka 23 amenyakua tuzo hiyo kwa Wachezaji wachezao ndani kwa kuzoa Pointi 127 akiwaangusha Mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Kipa Robert Muteba Kidiaba, aliepata 88 na Mchezaji wa Algeria, Baghdad Bounedjah aliyeambulia 63.

Nyota huyo anakuwa mtanzania wa kwanza kupata mafanikio hayo na sasa yupo mbioni kutua nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk ambayo imearifiwa tayari imekwisha kubaliana na nyota huyo.

Kwa upande wa tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wachezao soka nje ya Afrika, mchezaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, anayechezea Borussia Dortmund, alimbwaga Yaya Toure wa Ivory Coast na Man City baada kuzoa pointi 143 zikiwa 7 zaidi ya Toure ambaye alitwaa tuzo hii mara 4 mfululizo huku Andre Ayew wa Ghana akipata 112 na kumaliza nafasi ya 3.

Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast huku kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon huku tuzo ya klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo.

Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo, mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon naye mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364