-->

Samatta Azidi Kutikisa Nyavu Ulaya

Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Ally Samatta nyota yake imezidi kung’ara baada ya kuifungia klabu yake ya KRC Genk bao dhidi ya Club ya KV Oostende katika ligi kuu ya Belgium Pro League.

Samatta-45

Samatta alifunga goli hilo dakika ya 24 ambapo ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika kikosi cha kwanza (first eleven) katika timu hiyo.

Samatta alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu katika mechi hiyo dakika ya 24 akifuatiwa na Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya 81 na Camargo dakika ya 88 wakati Club ya Kv Oostende ilijipatia goli moja kupitia kwa Siani dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo timu ya KRC Genk iliibuka kidedea kwa bao 4-1 ambapo bao la Samatta ni bao lake ya pili tangu ajiunge na Club hiyo.

samatta-genk_1

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364