-->

Tupeni Uhuru Tufanye Yetu – Richie

Msanii wa filamu Tanzania ambaye juzi ameiwakilisha vizuri nchi na kutwaa tuzo nchini Nigeria Single Mtambalike au Richie, ameiomba serikali kuwapa uhuru katika kazi zao ili wapate uhalisia wa matukio.

RICHIE

Akiongea kwenye kipindi cha WeekendBreakfast juma pili kinachorushwa na East Africa Radio, Richie amesema kitendo cha wasimamizi wa kazi za sanaa kufungia baadhi ya kazi kwa kigezo kuwa hazina maadili zinawashusha kisanaa, na kupoteza uhalisia wa matukio.

“Watupe uhuru ili tupate uhalisia, unajua sio kila bongo movie unaangalia na familia,wanachotakiwa wao ni kuweka tu grade tu, hii ya miaka 18, unajua hii ni kazi lakini pia ni biashara, kama ni biashara lazima tuende kisasa ili kuleta uhalisia wa matuio”, alisema Richie.

Pia Richie amesema kitendo cha kukosa kuchaguliwa kwa filamu zake kuingia kwenye kinyang’anyiro hapa nyumbani kilimkatisha tamaa, ingawa alikuwa anajiamini katika utendaji wa kazi zake, na hatimaye kuweza kufika kimataifa.

“Tuzo za tanzania haikupita hata kuwa nominated, lakini kule wanakaa majaji wanaojua filamu, ya kwangu iliingia kategory mbili, niliamini najua kuandika, na niliamini nimejudgiwa na majaji waliobobea, ila mwanzo ilinikatisha tamaa na kujiona siwezi”, alisema Richie.

Pamoja na na hayo Richie pia amesema mwanzo hakuwa anapenda kuwa muigizaji, ila aliingia kwa lengo la kumsaidia rafiki yake Bishanga, lakini anaishukuru ITV kwa kumlea na kumfundisha mpaka leo anakuwa muigizaji bora.

“Mwanzo sikuwa napenda kuigiza, niliingia kwa kumsaidia Bishanga, niliingia nikiwa sijui kabisa, nafuata maelekezo, ukishakubali kuwa hujui basi utajifunza, na mpaka leo nimesimama nimelelewa kwenye misingi mizuri, watu wa ITV wamenifunza”, alisema Richie.

Pia Richie amesema kigezo kikubwa ambacho filamu yake ya Kitendawili kuweza kuchukua tuzo ya filamu bora ya Kiswahi ni maudhui yaliyo ndani yake, na uhalisia ambao unahusu maisha halisi ya Mtanzania.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364