-->

Shamsa Danga Ampongeza Dkt. Magufuli

shamsa-Danga

MSANII wa filamu wa kike na mtangazaji wa televisheni Shamsa Danga amempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli baada ya kuangalia tasnia ya filamu na muziki kwa kuwaimiza mamlaka ya Mapato kukamata kazi ambazo hazina stempu za ushuru wa mapato hasa zile za kutoka nje.

“Nampongeza mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa tamko kwa mamlaka ya Mapato TRA kuwabana wezi wa kazi zetu kwani hali imekuwa mbaya sana kwa filamu za kitanzania baada ya sinema kutoka nje kuuzwa bila kulipia ushuru na sisi kubanwa tulipe,”

Shamsa ambaye ni mtangazaji katika kipindi cha Dangache kinachorushwa Channel Ten amefurahishwa na kauli ya Rais aliyoitoa wiki iliyopita alipokutan ana baadhi ya wasanii wa muziki na Filamu Ikulu na kuagiza mamlaka ya mapato ifanye ukamataji wa kazi haramu (Fake) hasa zile za nje ambazo zimeua soko la filamu za Kibongo huku zikiuzwa bila kulipa ushuru.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364