-->

Ney wa Mitego: Muziki Sio Vita, Avunjiwa Vioo vya gari

Msanii Ney wa Mitego amepata ajali ya kuvunjiwa kioo cha gari yake na watu wasiojulikana, alipokuwa njiani akielekea EATV kwenye mahojiano ya kipindi cha Friday Night Live.

NAY98

Kwenye ukurasa wake wa instagram Ney wa Mitego ametoa taarifa hiyo, na kuwaomba radhi mashabiki wake kwa kushindwa kufika kwenye kipindi hicho, ambapo alitarajiwa kwenda kutambulisha video yake mpya.

“Nimevunjiwa kioo cha gari nikiwa njiani naenda kwenye Interview Chanel5 EATV, kwa ajili ya kutambulisha my new video, sorry watu wangu mliokua mkisubiri kuona video Na interview yote, nimeshindwa kufika naweka sawa hili, video itaenda YouTube kesho itakua kwenye Tv yako Pendwa”, aliandika Ney.

Pamoja na hayo Ney amewaonya watu wengine kuwa muziki sio vita, na kamwe hatoacha kufanya kile anachofanya kwa vitisho vyao.
“Muziki sio vita….. I will never stop doing what i do.!!” aliandika Ney.

NAY21

Hivi karibuni Ney wa Mitego alisema amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu tofauti tofauti baada ya kuachia wimbo wake wa shika adabu yako, ambao hata hivyo umefungiwa na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kutokana na uvunjifu wa maadili.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364