-->

Siataki Kulazimisha Umaarufu-Diana

MOJA ya changamoto kubwa inayowakabili baadhi ya mastaa nchini ni kushindwa kuwa na mfumo unaoendana na nafasi zao, kisa umaarufu na kujikweza kupindukia.

Lakini mwigizaji Diana Kimaro, anayeigiza filamu na Elizabeth Michael ‘Lulu’, amefichua kuwa hapendi kuanika mambo yake hadharani, akikiri ni mtihani kwake.

“Sitaki kufanya ‘interview’ kwa sababu sitaki kulazimisha umaarufu, sipendi kuandikwa andikwa kwa sababu nipo bize na kazi zangu, hata sasa naongea na wewe kwa heshima tu,” alisema.

Alisema kwa sasa anaye Meneja anayemwongoza kufanya chochote ili kuendelea kumjengea heshima.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364