-->

Shilole Afungukia Watoto Wake Kuimba

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amesema watoto wake hawana mpango wa kurithi kipaji chake cha uimbaji.

Akizungumza na MTANZANIA, Shilole alisema amekuwa akiwalea watoto wake katika maadili mazuri na kuhakikisha wanapata elimu ambayo itawasaidia baadaye.

“Hakuna mtoto ambaye ameonyesha mwelekeo wa kurithi kipaji changu, wote kila mmoja amejiwekea malengo yake, yupo anayetaka kuja kuwa dokta.

“Nafarijika kwa kuwa watoto wangu wamekuwa na bidii sana kwenye masomo yao, hilo ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Shilole.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364