Shilole: Wanaume Suruali Sasa Basi
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kuanzia sasa hataki tena kuwa na mwanaume suruali, bali anahitaji mtu mwenye nazo, ndiyo maana ameamua kufanya kazi kwa bidii.
Akilonga na Risasi Vibes, Shilole alisema kuwa kwa sasa ameamua kukaa singo kwa sababu ameona hakuna faida ya kuwa na mwanaume asiye na kitu.
Kuhusu Nedy Music anayedaiwa kuwa naye mara tu baada ya kumwagana na Nuh Mziwanda, Shishi Baby alisema hana uhusiano naye wa kimapenzi, isipokuwa ni rafiki wa kawaida tu!
Chanzo:GPL