-->

Lulu Awashukia Wanaoshindania Uzuri na Makalio

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael alimaarufu kama Lulu amefunguka na kusema kama wasanii wa filamu nchini wana wakati mgumu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo ya filamu nchini.

LULU23

 

Kupitia Account yake ya Twitter Lulu Michael ameonyesha kukatishwa tamaa na mambo mbalimbali kwenye tasnia hiyo huku akionyesha wazi uelewa mdogo na kukosa maarifa kwa baadhi ya wasanii ndiyo chanzo kushindwa kusonga mbele kwani wengi wao wanashindana kwa mambo ambayo hayana tija kwenye tasnia hiyo.

Lulu Michael ametamani kuongeza elimu zaidi ili aweze kushindana na watu wenye elimu zao na watu ambao watampa changamoto za ushindani katika mambo ya maana kuliko kwenye tasnia hiyo ambapo watu wana kazi ya kushindana kuvaa, uzuri na umaarufu.

“Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo outings na umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao mpya full kukatakata, hebu nikazane kusoma nianze ligi za kikubwa na dada zangu Wenye ma degree na ma masters Kama Esilovey hizi ligi nyingine zinasikitisha, watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo Outings na umaarufu, umaarufu wenyewe Kama network ya mtandao unaokuwaga mpya, full kukatakata,” aliandika Lulu Michael.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364