-->

Bifu la Shilole na Vanessa, Shilole Atangaza Vita

Msanii Shilole ametangaza vita na msanii mwenzake Vanessa mdee, na kusema kuwa asiombe kukutana naye popote.

SHILOLE546

Akiongea na East Africa TV baada ya kupigiwa smu kujibu tuhuma hizo, Shilole amesema amechukizwa na kitendo cha Vanessa kuandika mambo mabaya juu yake na kupost istagram, hivyo ajiandae kwa lolote.

“Ukiona hivyo ujue kimenuka, kaniongelea shit mi sijapenda, tena mwambieni nikikutana naye atanyooka”, alisema Shilole na kukata simu.

Hapo awali ilisambaa post kweny instagram iliypostiwa na Vanessa Mdee akimshambulia Shilole, na ndipo Shilole akapost na video kabisa akisema asioombe akutane naye kwani vibao vyake havielezeki.

Vanessa34

shilole43

Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’

“Vanessa nimepata ujumbe wako wa Kiingereza japokuwa nimeusoma kwa tabu sana lakini nimepata baadhi baadhi,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

“Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol,” anaonya Shishi.

“Aisee bibi, bibie, bibie, I am telling you yaani usiombe kukutana na Bi Shishi, yaani usiombe ukakutana na mimi tit for tat, yaani mama Kiingereza chako nimekiona, jipange, I am telling you, If I see you, me and you.” Shilole alimaliza

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364