-->

Shishi Baby Sasa Kwenda Kimataifa

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed ‘Shilole a.k.a Shishi Baby’, amesema kuwa kwa sasa ameweka mambo mengine pembeni na kuelekeza nguvu zake katika maandalizi ya kufanya ‘kolabo’ na wasanii wa kimataifa.

shilole78

Alisema kwa sasa hana muda wa kuzungumzia mambo mahusiano ya kimapenzi zaidi ya muziki ambao ni kazi aliyochagua kuifanya ili kuendesha maisha yake ya kila siku.

“Wapo watu ambao wamekuwa wakinipigia simu kunihoji mambo ambayo kwa kweli sina muda nayo kwa sasa, ila ninapenda niwaambie kuwa nimeelekeza nguvu kwenye muziki ili kufanya ‘kolabo’ na wasanii wa kimataifa,” amesema Shilole.

Nyota huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nuh Mziwanda ambaye tayari wamemwagana na kila kuchukua ‘taimu’ zake.

Msanii huyo aliwahi kutoa tangazo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akitafuta mwalimu wa kumfundisha lugha ya Kiingereza, kwa madai kwamba anajiandaa kufanya ‘kolabo’ na Nick Minaj.

Lete Raha

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364