-->

Sikumjua Nay mtu wa aina gani – Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa moja ya sababu yeye kuachana na mpenzi wake Nay wa Mitego ni kutokana na ukweli kwamba yeye hakutambua toka mwanzo kuwa msanii huyo ni mtu wa namna gani.

shamsaford23 (1)

 

Akizungumza kwenye kipindi cha Enews Shamsa Ford anasema wakati anaanza kutoka na Nay wa Mitego hakutambua ni mtu wa namna gani ndiyo maana aliweza kuanza naye mahusiano lakini kadili siku zilivyokuwa sikienda akagundua kuwa wana tofauti kubwa kwani tabia zao zilikuwa zikipishana sana.

Shamsa Ford alizidi kueleza kuwa awali alikuwa anaficha kama wanatoka kimapenzi na msanii huyo kutokana na ukweli kwamba kila mmoja alikuwa hana uhakika na mwenzake ndiyo maana walikuwa wanaitana “Cousin” ili hali wao ndiyo walikuwa wanajua ukweli kwamba ni wapenzi.

Mbali na hilo Shamsa Ford alisema baadaye aligundua kuwa akiwa ni mshikaji tu na Nay wa Mitego wanakuwa wanaelewana zaidi kuliko kuwa wapenzi ndiyo maana walifikia hatua kuachana na kuwa washikaji. Kwa sasa anasema amepata mpenzi mwingine ambaye ana sifa zaidi na wanapendana sana.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364