-->

Sina Mahusiano na Nisha – Baraka da Prince

Msanii Baraka da Prince amekanusha vikali kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Salma jabu au Nisha, kama tetesi zilivyozagaa mitandaoni.

NISHA BARAKA

Baraka da Prince amefunguka hilo kwa mara ya kwanza ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa msanii huyo ni rafiki yake wa kawaida tu.

“Mi siko kwenye mahusiano na sijawa tayari kuzungumzia mahusiano yangu, Nisha mi rafiki yangu bwana, ni mtu ambaye nipo nae muda mwingi, sina mahusiano yoyote na Nisha”, alisema Baraka.

Baraka da Prince aliendelea kusema habari hizo zimeanzishwa na mashabiki ambao kwa kuwaona pamoja wanadhani wana mahusiano.

“Mashabiki ndio wanatengeneza ile kitu, unajua mashabiki wa Tanzania wakiona mtu ukiwa famous ukionekana na mtu yeyote unaonekana una mahusano nae, mi ni mtu ambaye nishasingiziwa sana, nimedate watu wengi katika industry lakini sio kweli”, alisema Baraka de Prince.

Pia Baraka ameweka wazi kabisa suala hilo sio kiki ya kazi zake, isipokuwa ndio ukweli wenyewe.

“Haina kiki ile, kwani ushaona nimepost chochote about Nisha? Mi sidhani kama mapenzi yanale kiki aisee”, alisema msanii huyo kutoka pande za ‘rock city’ Mwanza.

Eatv.Tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364