Sipendi mwanaume mfupi -Tausi Mdegela
Msanii wa filamu nchini Tanzania na kipenzi cha watoto, Tausi Mdegela amefunguka na kudai urefu wa muimbaji wa taarabu Prince Amigo ndio kitu pekee kilichoweza kumchanganya mpaka kufikia hatua ya yeye kukubali kuolewa mke wa pili.
Tausi amebainisha hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali la miongoni mwa mashabiki zake waliotaka kufahamu ni kitu gani kilichomvutia kwa Prince Amigo na mpaka kuwa mpenzi wake.
“Napenda mwanaume mrefu mwembamba, sio mnene. Sipendi mwanaume mfupi, mfupi wa nini sasa tukiwa wote wafupi nani atazima taa, nani atafunga mlango”, amesema Tausi.
Aidha, Tausi amesema hatokubali kuona mtarajiwa wake huyo endapo atamuoa yeye kama walivyokubaliana aongeze mke wa tatu.
“Huyu ni muislamu sheria zinamruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja ila mimi nataka tuwe wawili tu, kwa sababu yule mke mkubwa ni mrefu, mimi mfupi. Anataka nini tena, sitaki aongeze mwingine wawili tunatosha”,amesisitiza Tausi.
Kwa upande mwingine, Tausi amedai yeye na mke mkubwa wanapata vizuri tofauti na watu wanavyofikilia mpaka kufikia hatua wanavaa nguo sare.
eatv.tv