-->

Zari saa chache baada ya picha ya Hamisa na videographer wa Diamond

Baada ya muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto kufikishana Mahakamani wiki iliyopita inadaiwa kuwa mambo yao yapo sawa kwa sasa na wamemaliza tofauti zao, hiyo ni baada ya kusambaa kwa picha za official videographer wa Diamond Platnumz ambaye ni Lukamba kusambaa kwa picha mtandaoni akiwa na Hamisa.

Kitendo cha Lukamba kuonekana kumfanyia photoshoot Hamisa kimeanza kuhusishwa kuwa Diamond na Hamisa wapo sawa kwa sasa ndio maana Lukamba ameonekana akifanya kazi za Hamisa ambaye ni mzazi mwenza na boss wake Diamond Platnumz.

Baada ya muda kupita baada ya picha ya Hamisa na Lukamba kusambaa mtandaoni Zari alipost ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram story na kuandika “Nafukuzana na pesa sio binadamu” ujumbe ambao unadaiwa kuwa amepost baada ya kuona picha ya Lukamba na Hamisa wakiwa pamoja kitu ambacho kinadaiwa kuzidi kuyumbisha penzi na Zari na Diamond na indaiwa kuwa bado hawapo sawa kwa sasa.

 

HARUSI YA SIRI YA AY, Zifuatazo ni picha kadhaa za kwenye harusi.

 

 

Comments

comments

Post Tagged with , , ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364