-->

‘Siri ya Mtungi’ Imenifungulia Milango Mingi-Duma

Msanii wa filamu Daudi Michael Tairo, anayefahamika zaidi kwa jina la Duma ndani ya tamthilia ya Siri ya Mtungi, amefunguka na kueleza jinsi tamthilia hiyo ilivyompatia mashavu ndani na nje ya nchi.

duma034

Mwigizaji huyo ambaye hapo awali aliwahi kushiriki katika filamu ya ‘Money Desire’, ‘Its Too Lets’ na filamu nyingine nyingi, ameiambia Bongo5 kuwa tamthilia hiyo ambayo ilikuwa ikionyeshwa katika runinga ya ITV na Channel Ten ndio iliyomfungulia njia ya mafanikio katika uigizaji.

“Tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ imenifungulia milango mingi sana na ndio tamthilia ambayo naiheshimu kwa kunifungulia milango ya kitaifa na kimataifa,” alisema Duma. “Ilinifanya nikapata deal Kenya na kuigiza kwenye tamthilia ambayo tayari imesharuka, kwa hiyo naweza kusema ni tamthilia ambayo imenipatia jina ambalo kwa sasa ndo nalitumia kama brand na hakuna mtu yeyote ndani ya bongo movie ambaye analitumia,”

Pia mwigizaji huyo amesema tasnia ya filamu kwa sasa inaushindani mkubwa hali ambayo inawafanya wasanii kuandaa kazi nzuri ili kuweza kufanya vizuri.

Mwigizaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na filamu yake mpya iitwayo ‘Mchongo sio’.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364