Goodluck Gozbert Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake
Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa nchini, Goodluck Gozbert akanusha kuonekana akijivinjari na mwanamke yeyote kwa sasa na kusema muda ukifika wa yeye kuwa kwenye mahusiano basi atakuwa.
Akiongea na eNewz, Gozbert alijibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na uvumi wa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akionekana na mwanamke wakijiachia naye na kudaiwa kuwa ndiye mpenzi wake ambapo alikanusha.
“Sina mwanamke kwa sasa na maneno ya watu yasikuchanganye, Ikifikia wakati wa Mungu kwa mimi kuwa kwenye mahusiano basi nitakuwa kwenye mahusiano ya ndoa” alisema Gozbert.
Hata hivyo Goodluck aliendelea kusema kuhusiana na muziki wa injili kuwa ni aina ya muziki ambao hauhitaji kiki kwa hiyo siku atakapokuwa tayari kwa swala la ndoa ataweka wazi kwa jamii inayomzunguka.
eatv.tv