-->

Sisi Tumebadilisha Muziki – Ferouz

Msanii Ferouz amesema utofauti mkubwa uliopo kati ya Bongo fleva ya zamani waliokuwa wanafanya wao na Bongo fleva ya sasa hivi, ni kwamba wao walikuwa wanaimba ujumbe wenye kuelimisha zaidi.

ferouz

Ferouz amyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV na kusema kuwa kitendo hicho kiliwahamasisha hata wasanii wachanga kufuata nyayo zao.

“Sisi wakati tunafanya muziki tulibadilisha muziki ukawa wa kuelimisha, tukaweka elimu na stori ndani yake, hata wasanii waliokuwa wanachipukia wakawa wanasema ok nikiimba kama fulani inabidi niimbe kitu chenye ujumbe,” alisema Ferouz.

Ferouz ambaye ameanza gemu ya muziki kitambo, amesema yeye binafsi akishaimba wimbo hategemei sana kufanya video kali, kwani ujumbe wa kwenye wimbo ndio muhimu, na video huwa anafanya tu kuupa heshima huo wimbo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364