-->

Snura Akanusha Kufungiwa Yeye na Wimbo Wake

Baada ya taarifa kuenea kuwa Snura amefungiwa kujihusisha na kazi ya sanii nchini pamoja na wimbo wake na video msanii huyo amepaza sauti yake na kusema kuwa yeye hajafungiwa kufanya sanaa wala wimbo wake haujafungiwa na serikali.

snura145

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Snura amesema kuwa katika barua ambayo alipewa imeeleza wazi kuwa video ya wimbo wake huo ‘Chura’ ndiyo imesitishwa kwa muda mpaka hapo atakapofanya video nyingine yenye maadili na kusema watu wanaosema kuwa yeye amefungiwa kujihusisha na sanaa ni wapotoshaji na waongo.

“Hata Serikali ikiona itaona waandishi kama mnasema uongo kwani sijafungiwa mimi kufanya kazi ya sanaa bali wimbo wangu umesitishwa mpaka nifanye video nyingine nzuri, hivyo mimi sijafungiwa, wala wimbo hajafungiwa hiyo kitu tangia jana wao ndiyo waliiweka hivyo, kwani hata katika copy ya barua ambayo mimi nimepata inasema hivyo na barua nyingine ilipelekwa kwa waziri ndiyo maana nikiona mtu anadanganya nakuwa sipendi” alisema Snura.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364