-->

Soba Wazungumzia ‘Ubwiaji’ wa Chid Benz

Ni wiki kadhaa tangu mkali wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ apelekwe kwenye Kituo cha Life & Hope Rehabilitation Organization (Soba House) kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kupata huduma ya kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya.

chid
Chid Benz alipelekwa kwenye kituo hicho chini ya uangalizi wa Promota, Babu Tale kufuatia hali yake kuwa mbaya kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kwa muda mrefu.
Kituo hicho kina jumla ya waathirika 33 wa dawa za kulevya, bangi, pombe na kadhalika. Waathirika wanapofika kituoni hapo wanapata ushauri wa kitaalam, malezi ya namna wanavyoweza kupambana na kuacha kutumia dawa hizo pamoja na mafundisho ya kiimani.
Showbiz Xtra ilifanikiwa kutinga katika kituo hicho ambapo siku hiyo Chid alipelekwa katika vipimo hivyo aikuweza kuonana naye. Hata hivyo, ilifanikiwa kuzungumza na meneja msaidizi wa kituo hicho ambaye naye aliwahi kutumia dawa hizo, Said Aman na wengine ambao ni waathirika wa madawa wanaolelewa kituoni hapo waliomzungumzia Chid.

Said Aman
“Mimi ni msaidizi wa kituo, awali nilikuwa mwathirika wa dawa kwa miaka minne. Niliingia kwa sababu ya kampani mbaya lakini nilipojitambua na kutaka kuacha ndiyo nikaja hapa, kwa sasa nimepona kabisa na hata kwa Chid kama ameamua mwenyewe na siyo kwa kulazimishwa basi atapona,” anasema Aman.

Khalim Joseph
“Nina familia ya watoto watano, mimi ni mwathirika wa pombe, kutokana na mishe zangu kutokwenda vizuri niliamua kunywa sana nikiamini napunguza mawazo kumbe nazalisha tatizo lingine.
“Nimepoteza muda, nilisemwa na kutengwa na jamii lakini kwa miezi sita niliyokaa hapa kituoni nimekuwa mtu mwingine, nilikuja na uzito wa kilogramu 70 sasa nina 85. Namshauri Chid kama  mdogo wangu inawezekana kubadilika na kuachana na unga,” alimaliza Khalim.

Said Nassoro
Nilikuwa na watoto wawili ila mmoja nilimpoteza kwa sababu ya uzembe na malezi mabaya kutoka na miaka 10 ya matumizi ya unga na pombe kali.
“Inaniuma kumpoteza mwanangu kwa uzembe, ndugu zangu wanisamehe na kwa sasa niko vizuri na ninamshauri Chid kuwa anaweza kujitoa katika shimo hilo la uteja na kufanya kazi zake za sanaa,” anasema Said.

Sultan Fikirini
“Chid anatakiwa kuelewa kuwa mwanzoni atapata kipindi kigumu cha kulipa alosto kutokana na maumivu makali sana, kutapika, kukosa usingizi na mengineyo. Ila baada ya hapo atarejea katika hali yake ya awali ila namuona yuko vizuri darasani na kazi zingine.

Rashid Amo
Tunamuomba Rais wetu John Pombe Magufuli azidi kukaza hasa kwa wanaotumia na wanaoingiza dawa, kwani  zinatuharibu na kumaliza sana vijana ambao ni nguvu kazi.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364