TAFF Imeunganisha Tasnia ya Filamu
SIKU za nyuma kulikuwa na malumbano makali kati ya shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) na kundi la Bongo Movie Unity lilokuwa likiundwa na wasanii nyota katika tasnia ya filamu Swahilihood na kuleta sintofahamu .
Lakini kutokana na juhudi za Mwakifwamba pamoja na makamu mwenyekiti wake Deosonga Njerekela wamefanikiwa kuwaunganisha na sasa ni kundi moja wanaongea lugha moja kufuatia vikao vya upatanishi vilivyofanyika miezi ya awali mwezi wa kwanza hadi wa pili Taff inapata nguvu zaidi baada ya kuwapa nafasi na wasanii kutoka Bongo movie kushika hatamu za uongozi na kuwa sasa ni shirikisho kamili lenye sura zote hongera.
Tarehe 25. February .2016 ni siku muhimu sana ya kukumbukwa kwa wanatasnia ya filamu baada ya kuandika historia kwa kufanya uchaguzi mkubwa sana huku zaidi ya mikoa kumi na saba kushiriki uchaguzi kwa wanachama wote kuja Dar es salaam kupiga viongozi wao
Viongozi waliochaguliwa kugombea nafasi za ujumbe wa bodi na vyama vya wasanii vinavyounda Taff mkutano ulikuwa na ushindani sana hasa nafa za kitaifa na mikoa huku nafasi ya urais ikionyesha kuheshimiwa zaidi baada hata aliyekuwepo hadi mwisho kuamua kujitoa na kumwacha Kingunge Mwenyewe Mwakifwamba kugombea na hiyo na kupigiwa kura zote za ndio 49 kati ya kura 52 Kura tatu zikiharibika na kumfanya aibuke kwa kishindo na kumshukru Mungu huku pia watu wote waliompigia kura na waliomuunga mkono kwa kila hatua na kumfanya awe mshindi nafasi ya urais Mwakifwamba aliingia katika kinyanganyiro hicho pekee baada ya mpinzani wake Issa kipemba kujitoa.
Makamu mwenyekiti Deosonga aliingia toka awali akiwa pekee yake na kuibuka kwa ushindi wa asilimia 98.04 baada ya kukosekana mpinzani kwani nafasi hiyo ilikuwa ni ngumu kwa wasanii wengi kwani makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Katiba ya Taff ndio kiungo cha vyama vyote, ndio mratibu wa mahusiano ya kimataifa hivyo inahitajika mtu mwenye uzoefu wa shughuli za kimataifa hivyo uzoefu pia ni moja ya kigezo kuwa na uzoefu wa shughuli kimataifa.
wajumbe waliopita ni pamoja na Adam Juma, John Kallaghe, Juma Chikoka, Ummy mohamed, Michael Sangu, Single Mtambalike, Kimu kutoka Mwanza, Dada Irene Sanga, Ali Baucha na wengine hawa ni wajumbe wa Bodi ya Taff.
awali nilisema kuwa kumekuwa na muunganiko mkubwa kwani kuna vyama kama chama cha watayarishaji mwenyekiti ni William Mtitu, huku chama ambacho ni muhimu sana cha waongozaji kimechuliwa na Vincent Kigosi maarufu kama Ray, huku nafasi ya makamu ikienda kwa Chrissent Mhenga baba wa wasanii wengi waliotokana na kundi la Kaole,
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa habari Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh. Nape Nnauye na kuwaasa wasanii akiwaambia yupo kwaajili yao na wachague viongozi wachapa kazi na si wale wanaotaka Cv tu kwa ajil ya mambo yao kwani maharamia wa kazi za wasanii
wanaojinufaisha kwa ajili ya jasho la wasanii wapo wengi na wana nguvu kama wakiwekwa viongozi legelege vita vitakuwa vigumu japo ushindi utapatikana lakini kwa nguvu nyingi sana hivyo wampe viongozi wachapakazi bila uonevu wala upendeleo.
“Napenda kuahadi nifanya kazi nanyi kwa nguvu zote hata kama nikikaa kwa miaka miwili ningepend a niwaachie kitu kikubwa ambacho hamtakisahau katika historia ya uwepo wangu kama waziri katika wizara inayowahusu na kama waziri wenu, ni kijana mwenzenu nina nia thabiti ya kuwatoa huko,”
Waziri amesisitiza kuwa lazima viongozi wajitoe katika kusimamia maslahi yao kwa kutouza haki zao kwa watu wasiovuja jasho na kujikuta ni watu wa kulalamika kila siku, naye Rais mteule Mwakifwamba baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi alisema ana vipaumbele vinne muhimu.
“Kwanza nimshukru Mungu na jamaa wote waliojitoa na kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika salama na kuwapata viongozi safi, nina vipaumbele vinne 1. Elimu, 2.soko la filamu,3 mfuko wa wasanii na tamasha kubwa la Filamu,”
Uchaguzi huo ulishirikisha pia viongozi wa kiserikali Bi. Joyce Fissoo katibu wa Bodi ya ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza, katibu wa Basata G. Mwingereza.