-->

Thea Atetwa kwa Vimini, Acharuka!

MSANII mkongwe wa fi lamu Bongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amejikuta akitetwa akidaiwa kuwa mcharuko kwa kuvaa vimini hasa baada ya kuachana na mumewe, Michael Sangu ‘Mike’.

THEA34

Kutetwa huko kumeonekana kumkera sana Thea ambaye juzikati akichonga na Ijumaa alisema, anawashangaa wanaomsema vibaya kwani anaamini anaishi maisha anayotaka yeye na wala hakuna anayeweza kumzuia.

“Mimi napenda kuvaa vimini tangu zamani na sasa hakuna anayenizuia kwani haya ni maisha yangu, nawashangaa sana  anaonisengenya yaani wananikera sana sijui  ananitafuta nini, siwezi kuwa mcharuko kwa sababu eti ndoa imevunjika  ama wanavyosema kwa sababu mimi ndiye niliyemuacha Mike hivyo wanikome,” alisema Thea.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364