-->

Tukumbuke Kuwa Haya Maisha Ya Duniani ni ya Kupita-Wolper

Kutoka kwenye ukurasa wake mtandaoni,nyota wa bongo movies, Jacqueline Wolper ametukumbusha hili.
wolper23

Kuna wakati tunatatakiwa tujue na tukumbuke kuwa haya maisha ya duniani ni ya kupita kuanzia binadamu pamoja na vitu vya duniani. Binadam tunajisahau sana tunawaza kutafuta mapesa na magari ya kifahari na majumba ya kifahari lakini hatujipangi kutafuta maisha ya huko tuendako yani kaburini??.

Wengine wanagombaniana maviwanja na kudhurimiana viwanja lakini siku ya kuzikwa tunachimbiwa kasehemu kadogo tu na ndo mwisho wetu unaishia hapo???Ee Mungu najua mm ni mkosefu na ninajua na kukwaza na kuishi kinyume cha amri zako wakati mwingine ila naomba uzidi kunitia hofu yako na maisha ninayoelekea na kila siku nijue hapa duniani sio kwangu kabisa na pia nijue mbinguni hakuna ustar wala uraisi,haya ya ustar na mengine ni mapito ya dunia kwako haya mambo hakuna?Yanii hakuna kabisa kwa sababu ww hukuumba mtu wa kumzidi mwenzie ww ulitumia wote sawa ingawa duniani tunakosoana mwingine anamuona mwenzie sie yeye ndo anajiona ndie lakini mwisho wa siku wote tunaishia sehemu moja daaah.

Embu tukumbuke hizi Mali tutaziacha zoteee na warithi pia wataziacha hakuna mwenye chake hapa duniani kama ulivyozaliwa bila gari ndo utakufa hivyo pia…Leo utaiba Mali ya mtu lakini kumbuka na ww utakufa kesho utaroga mtu jiulize utaishia wapi..ww ulie chini na ww ulie juu sisi wote tumembwa na Mungu na tumezaliwa na tutakufa vya dunia vina mda wake tujitahidi kujipanga kwa ajili ya maisha yetu ya kaburini na sio maisha ya duniani.

Kitu kingine ata watukanaji wa insta pia mnatakiwa mkumbuke na nyie mtakufa na hizi insta tutaziacha na wakati ukifa utaaacha kumbu kumbu yako ya matusi…Embu tumuogope Mungu na tufikirie maisha yetu ya tuendako pia tumejipangaje???

Wolper on Instagram

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364