-->

Ukipata Mtu Kama Riyama Usichelewe Kumuoa – Leo

Leo Mysterio ambaye ni mchumba wa malkia wa filamu nchini Riyama Ally amefunguka na kusema “unapopata mtu anayestahili kuwa mke usicheleweshe kufanya maamuzi ya kumuweka ndani”.

riyama19

Leo Mysterio amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwa sasa tayari yeye amefanya maamuzi ya kuishi na Riyama na muda wowote kuanzia sasa wanaweza kufunga ndoa kwani hatua za awali tayari wameanza kuzifanya.

“Unajua Riyana ni mtu ambaye ana huruma sana, ana akili pia ana mapenzi ya kweli kwangu na amekuwa akinisaidia katika kazi zangu hivyo nimefikia wakati nimeona ni bora nimuweke ndani kwani nimeridhika na yeye kwa kila kitu, ndiyo maana sijataka kuchelewesha kwa sababu yeye ndiye mwenye sifa kwangu” Alisema Leo Mysterio

Mbali na hilo Leo Mystereo amesema hajakurupuka katika maamuzi sababu yeye tayari alishafahamiana na Riyama Ally kwa zaidi ya miaka kumi uliyopita, lakini pia hajawahi kumuweka wazi mpenzi wake yeyote yule kipindi cha nyuma lakini mpaka amefikia hatua hii amejiridhisha na kuona kuwa Riwaya ndiye chaguo lake la kweli.

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364