-->

Ishakua Soo Itamembeba Niva- Jimmy Mafufu

Mafufu na Niva wakiwa kwenye moja ya scene za 'Imeshakuwa Soo'

Mafufu na Niva wakiwa kwenye moja ya scene za ‘Ishakuwa Soo’

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Bongo Jimmy Mafufu ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa filamu ijayo hajaona msanii wa Bongo wa kumshirikisha kwani wasanii wengi ameshawashirikisha katika filamu zake nyingi na sasa anaangalia uwezo wa kuwatumia wasanii wakubwa kutoka .

“Sioni tena msanii wa kumshirikisha filamu zangu za kiume maana katika filamu yangu ya Ishakua Soo nimemshirikisha kijana wangu Niva na hajaniangusha nafikiria ndio wa mwisho kucheza na mimi natamani kucheza na msanii kama Jason Statham,”anasema Mafufu.

Mafufu anatamba kwa kusema kuwa wapenzi wa kazi zake ambao wamekuwa wakiwataja wasanii wakali kama King Majuto, Riyama Ali na wengine tayari amewashirikisha katika kazi zake zilizopita na sasa anataka kuwatumia wasanii wa nje ya nchi kama ni hatua kuelekea kimataifa.
FC

Subscribe kwenye channel ya Bongo Movies TV kwenye Youtube ujionee video nyingi zaidi za Bongo Movies

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364