Uvumilivu Umemshinda Vanessa Mdee Kisa Jux
Msani wa bongo fleva Vanessa Mdee maarufu kama V Money ameshindwa kuvumilia baadhi ya Comments zinazotolewa na baadhi ya mashabiki wake kwenye account yake ya Instgram baada ya msanii huyo kumzungumzia mpenzi wake Jux.
Inafahamika kuwa wiki hii Jux atakuwa na show kadhaa katika mikoa mbalimbali hivyo mwandani wake Vanessa Mdee alichukua muda kumpa support Jux kwa kupost picha ikiwa imeambatana na maneno yaliyosomeka “Moro na Dodoma sio kwa kunichukulia mtu wangu weekend nzimaaaa dahhhhh!!! Freshi lakini nendeni mkashow love basi.” Aliandika Vanessa
Lakini kauli hiyo ilipokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wakidhani labda Vanessa Mdee amemaanisha kuwa anaogopa kuibiwa mtu wake, jambo ambalo liliwafanya watu waanze kusema kuwa yeye ndio amemuiba Jux kwani wao wanaamini kuwa Jux bado anampenda Jacky Clif ila kikwazo ni kwa kuwa Jacky yuko kifungoni China.
“Mwenye nacho yupo jela ila siku akitoka aibu kwako pole kwa kujitapa na Jux wa Jack ila malipo ni hapa hapa” aliandika Tangaloj
Lakini yupo shabiki ambaye alifanya Vanessa Mdee ashindwe kuvumilia na kuamua kumjibu tu, shabiki huyo yeye alisema kuwa Jux pamoja na Kamikaze si wasanii bali ni wababaishaji katika muziki jambo ambalo liliibua hisia hata kwa mashabiki wengine na kuanza kumchana shabiki huyo, lakini Vanessa aliweza kumwabia maneno haya.
“D.Magezi kwaresma yote hii usije ukanishindisha nja mwanangu naona kuna mengi yanakustress kama vipi Pita Left arifu isiwe tabu.” Alisema vanessa Mdee
Vanessa Mdee hakuishia hapo alitumia account yake ya Twitter kuonesha kuwa hajapendezwa na jambo hilo na aliandika hiki tena “Uko Instagram watu wakiona kitu kimewazidi basi mapovu yanawatoka dah! Ukisoma comments utadhani vita, ila tenda wema nenda zako, Mungu anaona achana na wanadamu” Aliandika Vanessa Mdee
eatv.tv