Ving’amuzi Vinaua Bongo Movie – Chekibudi
Star wa Bongo movi Chekibudi anaumizwa moyo na ving’amuzi kutokana na kwamba ni moja kati ya vitu vinavyoua kwa kasi soko lao la filamu.
Akizunguma na Enewz Chekibudi alisema kuwa ving’amuzi vingi vimetoka kwa sasa na vinaonesha filamu mbalimbali kitu kilichopelekea mauzo ya kazi zao kushuka.
“Sisi tulipotea pale tulipouza kazi zetu badala ya kuuza kopi lakini mtu anajifunza kutokana na makosa, kwasasa tunajipanga ili tusilifanye hilo tena”.