-->

Wake Zangu Wananivuruga Akili-Mzee Yussuf

Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yussuf amesema hakuna kitu kinamuumiza kichwa kama kutoelewana kwa wake zake wawili.

mzee4

 

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Mzee Yussuf amesema anapitia wakati mgumu sana kuwamiliki wake wawili anaowapenda wakati wao hawapendani.

“Kusema kweli napata wakati mgumu kuwahandle, yanii linanivuruga sana hili swala,” alisema Mzee Yussuf. “Ndio maana natamani hata kesho waelewane. Sometime ni raha wakiwa hawaelewani kwa maana hata kama nimeenda pahali labda nimezunguka hakuna anayelinda” alifafanua zaidi.

“Lakini hii ni chugu sana, hili kwangu ni tatizo, natakamani leo au kesho waelewane. Lakini tatizo la hawa yote ni watu wa karibu, ndio maana mimi nimeshawaambia kwa mdomo wangu, hili jambo nataka liishe, sitaki kusema naomba liishe kwa sababu nilishawaomba sana, na ninachoona ustaa ndio unawasumbua wanashindwa kujua mimi ni staa zaidi yao,” aliongeza Mzee Yussuf.

Mwanzo wa mwaka huu, Mzee Yussuf alidai wake zake Leila Rashid na Chiku awamekatazwa kutumia mtandao wa Instagram kwa madai mtandao huo unakuza ugomvi wao.

Bongo 5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364