-->

Wanigeria wamvimbia Diamond Platnumz kisa tuzo ya SoundcityMVP

Baada ya msanii wa muziki Diamond Platnumz kutoka Tanzania, kuibuka msindi wa tuzo ya muziki ya Soundcity MVP Awards 2017, kupitia kupengere cha ‘Best Male MVP’ wadau na mashabiki wa muziki nchini Nigeria wameonyesha kutofurahishwa na ushindi huo.

Katika kipengere hicho alichoshinda Diamond, alikuwa akichuana na wasanii kama Runtown, Davido, Olamide, 2face Idibia, Wizkid, Shatta Wale, Navio na Sarkodie.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mashabiki hao wameonyesha hisia zao za kutofurahia ushindi wa msanii huyo.

Ugawaji wa tuzo hizo umefanyika usiku wa jana nchini Nigeria na msanii Davido aliibuka kinara kwa kutwaa tuzo tatu kubwa ambazo ni ‘Song of the Yeara’, Video of the year’ na ‘African Artist of the Year Award’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364