-->

Wasanii Bongo Umoja Wetu ni wa Misibani Tu: Mtanga

Muigizaji wa kundi la Zecomedy la EATV, Mtanga amesema wasanii nchini hawana umoja kama watu wanavyodhani ila umoja huonekana pindi kukiwa na tatizo la msiba ndipo wasanii hukutana kwa umoja.

mtanga90

Mtanga

Mtanga ameyasema hayo kupitia kipindi cha SUPAMIX ‘Kamatia Kitaa’ ambacho kimefanyika katika stendi ya Morocco Jijini Dar es Salaam ambapo kundi la Zecomedy limejumuika na wananchi kujadili masuala mbalimbali ikiwemo umoja wa wasanii nchini.

“Hakuna umoja wasanii nchini, na tukikutana kwa pamoja ujue kuna msiba na ndipo watakuja wasanii mabimbali na suti zao kali na magari yao kuja kujionyesha mbele za watu, lakini kukaa pamoja kwa umoja na kupanga mikakati ya kuendeleza sanaa yetu na kusaidiana hilo halipo” Amesema Mtanga.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364