-->

Wasanii Watoa ya Moyoni Bajeti ya Sh Bilioni 3

WAKATI Serikali ikitenga Sh bilioni 3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo zitakazotumika kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Ubunifu, wasanii wa fani mbalimbali wameeleza mitazamo yao kuhusu bajeti hiyo.

jb657
Wasanii hao kwa mitazamo yao wamezungumzia namna ambavyo fedha hizo zimeelekezwa kusimamia urasimishaji wa shughuli za sanaa, kusimamia na kudhibiti filamu zitakazoingia sokoni bila kufuata taratibu na kuratibu uendeshaji wa kazi za sanaa nchini.

 Bongo Fleva

Mkali wa rap nchini, Afande Sele, alisema iwe katika utekelezaji badala ya kujaa maneno mengi kuliko vitendo, maana ahadi ni nyingi nchi hii bila vitendo.
“Mimi naomba utekelezaji uweze kubeba nafasi kuliko maneno hewa,” alimaliza Afande Sele.
Naye mkurugenzi wa kundi la Mkubwa na Wanaye, Said Fella, alisema ni kwa mara ya kwanza usimamizi wa kazi za wasanii umewekewa bajeti kikubwa kinachotakiwa uimarishwe ulinzi wa kazi za wasanii ili waweze kujipatia maendeleo kupitia kazi zao.
Stara Thomas alisema mwanzo mzuri kwa kuwa awali hali hiyo haikuwepo.
“Tumeangaliwa kwa jicho la huruma hivyo tujitambue na tuitumia vyema nafasi hii, pia upande wa wezi wa kazi zetu tutashukuru kama litafanyiwa kazi vizuri kwani wasanii wengi wamekuwa wakikata tamaa kutokana na kuibiwa kazi zao.”
Mwigizaji anayewakilisha wasanii wanaokuja juu kwa kasi, Da Zitta, alisema sanaa ni fani inayoingiza kiasi kikubwa cha fedha kupitia kodi lakini suala la kazi kuibiwa ndicho kitu kinachokwamisha wengi, pia upande wa manunuzi ya kazi zetu mpaka ujisimamie mwenyewe hili tatizo Serikali liliangalie sana na wasanii pia kwa pamoja tuweze kushikana mikono ili tuweze kufika hatua stahiki.

Waigizaji

William Mtitu, mwigizaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya 5 Effects, ameiomba Serikali kuhakikisha fedha hizo zinatumika kusaidia wasanii na kazi zao zisielekezwe katika semina na mikutano ya viongozi wa wizara.
“Kama fedha hizo zitaelekezwa kwa wasanii wenyewe zitasaidia na bajeti itakuwa na maana lakini kama zitatumika kwa vikao vyao bajeti haitakuwa na maana kwa wasanii, pia Serikali izuie filamu za nje katika soko la ndani ili filamu za ndani zipate soko la kutosha na kunufaisha wasanii wake,” alisema Mtibu.
Mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amesema: “Mimi naishauri Serikali itumie vizuri fedha ilizozitenga zifanye kazi katika vitengo husika na lengo ni kuboresha sekta ya sanaa ili zilete mabadiliko ya kimaendeleo kwa wasanii,” alieleza.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifamba, amesema: “Bajeti ni nzuri tunaomba ikabidhiwe kwa wizara mapema ili iweze kufanyakazi yake isibaki katika makaratsi tu, pia tunamshukuru sana waziri Nape kwa kujituma kwake na kutambua umuhimu wetu kama wasanii katika jamii.
Mzee Chillo amewaomba wasanii watambue kwamba fedha hizo ni kwa ajili ya maendeleo ya wasanii na si kwamba kila msanii atapata za kwake bali zitaleta mwanzo mzuri kuelekea kwenye mafanikio.
Jacob Steven (JB) alisema kazi kubwa iliyobaki ni kwa wasanii kujitambua na kutekeleza majukumu yao kama wasanii.

Wachekeshaji

King Majuto amesema sanaa kutengewa fedha ni jambo la kupongezwa kwa kuwa haijawahi kutokea ila ameomba fedha hizo zifanye kazi kweli isiwe kwa ajili ya kutufurahisha kisha wananufaika wengine.”
Naye Haji Salim maarufu Mboto amefurahishwa na bajeti hiyo na anaipongeza Serikali kwa kuona uwepo wa sanaa nchini, kwani tasnia ya filamu imekosa uangalifu na utetezi.
“Ehe! Tumekumbukwa, jamanii,” alijibu kwa kuchekesha.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364