Wasanii Wawili Wafariki Bongo Muvi
Misiba! Wakati wadau wa Bongo Movies wakiwa kwenye majonzi ya kifo cha Michael Dennis ‘John Woka’, kwenye Bongo nako kuna pigo la kuondokewa na wasanii wawili, Maneno Gongo ‘Mr Gongo’ na Jennifer Vincent ‘Mama Utajiju’.
Gongo alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu.
Marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, ndugu wa marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa, alisema kuwa msanii huyo alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda refu na alikuwa akijaribu kila dawa bila mafanikio.
Mchuwa alisema kuwa jamaa huyo alizidiwa hadi akakakamaa hivyo walimpeleka Muhimbili ambapo ndiko alikokutwa na umahuti.
Msanii huyo ambaye alizikwa kwenye Makaburi ya Visiga, Kibaha mkoani Pwani amecheza filamu mbalimbali zikiwemo The Mask akiwa na Aunt Ezekiel, For Sale, Stolen Gold, Sara na nyinginezo.
Wakati simanzi hiyo haijapoa, mwigizaji mwingine, Mama Utajiju yeye aliaga dunia kwa kuumwa ghafla.
“Nasikitika kuondokewa na msanii wangu mzuri kama mtakumbuka alifanya vizuri sana kwenye Filamu za Mwanavita, Nakufa kwa Ajili Yako na Yote ni Baba,” alisema mkurugenzi wa kundi hilo, Fatma Makame ‘Joanitha’.
Chanzo:GPL