-->

Ray C Afungiwa Hospitalini

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kuwekwa chini ya uangalizi maalum akiwa amefungiwa kwenye Hosptali ya Mwanayamala, Dar baada ya madai ya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’.

RAY C22

Chanzo makini cha Ijumaa Wikienda kilimshuhudia Ray C akiwa kwenye wodi maalum ya waathirika wa unga huku mama yake mzazi akiwa anamuangalia wakati wote.

Mpashaji wetu huyo alifunguka kuwa, kuna muda Ray C alitoka nje na kuanza kuongea maneno ambayo hayajanyooka lakini dakika chache baadaye alikuja muuguzi na kuanza kumtafuta kwa kumuita jina lake akihofia huenda ametoka nje ya geti.

“Jamani Ray C yupo hapa, anaonekana hayuko sawa kabisa kwa sababu ametoka hapa nje ya wodi ameanza kuzungumza vitu ambavyo havieleweki,” kilisema chanzo hicho.
Kilizidi kuweka wazi kuwa baadhi ya waathirika wenzake walikuwa wakimsema kuwa bado ameweka ustaa mbele, kitu ambacho kinamuharibia kwa kuwa hafuati masharti ya kutumia dozi hiyo ya kuacha unga ya Methadone.

Gazeti hili lilifunga safari hadi hospitalini hapa ambapo lilionana na daktari wa kitengo hicho (jina tunalo) ambaye alikiri kuwa mwanamuziki huyo yupo hospitalini hapo kwa matibabu.

“Kuna hali fulani inawapata sana wagonjwa wetu maana wanahitaji sana utulivu hivyo yuko hapa kwa ajili ya tiba na muda si mrefu atakuwa tena uraiani kama zamani, tunajitahidi kumtibu ili awe sawa,” alisema daktari huyo.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364