Wastara Atumia Mil 180 Kununua Mjengo
Huku kukiwa na madai mazito ya kumchuna aliyekuwa mumewe ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma, staa wa sinema za Kibongo, Wastara sasa anaripotiwa kununua mjengo wenye gharama ya Sh. milioni 180 za Kitanzania, Wikienda limechimba.
Pamoja na misukosuko yake na Sadifa, ubuyu kutoka kwa mtu wa karibu wa Wastara unanyetisha kuwa Wastara kwa sasa mambo yake ‘supa siyo dizeli’ kwani anaonekana mshiko umemtembelea na kununua nyumba hiyo iliyopo Gongo la Mboto, Dar.
“Jamani nawapa ishu lakini msinitaje, lakini ukweli ni kwamba Wastara amenunua nyumba maeneo ya Gongo la Mboto.
“Wapo wanaosema eti mbwembwe zote anazifanya na fedha alizomchuna Sadifa lakini pia wapo wanaosema kuwa nyumba hiyo amepangishiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Sanan kwani maeneo aliyonunua nyumba hiyo ndiyo anayokaa Bond,” alifunguka ‘kikulacho’ huyo.
Sosi huyo aliendelea kunyetisha kuwa, pamoja na kwamba Wastara kwa sasa yupo nchini Msumbiji kibiashara (anafanya biashara ya nguo) lakini nyumba hiyo wanakaa watoto wake.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye meza ya Wikienda, mwanahabari wetu alimtafuta Wastara kwa njia ya simu baada ya kuhakikishiwa kuwa hayupo Bongo, alipopatikana alikiri kununua nyumba kwa Sh. milioni 180.
Katika mahojiano ya Wikienda na Wastara, mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Wastara kuna madai kuwa umepangishiwa nyumba na Bond kwa sababu mmerudiana ingawa wapo wanaosema umeinunua, je, hilo likoje?
Wastara: Unajua watu wanapenda kunizushia lakini mimi sipendi. Huyo Bond sijarudiana naye bali ninaongea naye kwa sababu ya kazi (uigizaji). Kuhusu nyumba nimenunua mwenyewe.
Wikienda: Kuna madai mengine kuwa fedha ulizonunulia nyumba ulimchuna mbunge (Sadifa), wewe unasemaje?
Wastara: Kwanza mimi sikuona fedha ya kumchuna huyo mbunge na hakuna fedha aliyonipa. Mimi ni mfanyabiashara, biashara zangu za madini, nguo na urembo ndizo zinaniingizia fedha. Ifahamike kuwa nilianza kufanya biashara tangu kitambo.
Wikienda: Je, ni kweli umeuza nyumba yako ya Tabata? Au ni kwa sababu inatakiwa ibomolewe hivyo umeisusa?
Wastara: Sijaiuza, naikarabati, Mungu akipenda nitawaweka watoto yatima kwani ndiyo mipango yangu ya siku nyingi.
Sadifa alipotafutwa kwa njia simu ili kusikia kauli yake, hakuweza kupatikana hewani jitihada zinaendelea.
Chanzo:GPL