-->

Mabasi ya Haraka Kuanza Kutumia Gesi

Gazeti la Habari Leo limeripoti kuwa` msimamizi wa usambazaji gesi katika shirika la maendeleo ya petrol  Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama.

mabasi90

Kupitia gazeti hilo Naleja amesema matumizi ya nishati hiyo yataanza katika awamu ya pili ambapo mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongezeka idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na  kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

’‘Uendeshaji wa gesi utakua nafuu jambo linaloweza  kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi itatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu”

Millard Ayo.Com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364