-->

Wastara Auza Vitu Vyake vya Ndani

Inauma sana! Msanii wa filamu ambaye anasumbuliwa na tatizo na mguu, Wastara Juma inadaiwa hali aliyonayo kwa sasa si nzuri na kupata pesa ya matibabu imekuwa ngumu kwake hivyo ameamua auze baadhi ya vitu vyake vya ndani.

wastara788

Ndugu wa Wastara aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema kuwa, msanii huyo anapitia kipindi kigumu kwani anahitaji pesa nyingi ili arudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu.

“Kwa maumivu aliyonayo hapati hata muda wa kutoka, muda mwingi yuko ndani tu na ninavyoongea na wewe sasa ameanza kuuza vitu vyake vya ndani ili aweze kupata pesa za matibabu, si unajua anatakiwa kuwa na shilingi milioni 10 kabla ya kurudi Nairobi kwa matibabu mengine?” kilidai chanzo hicho.

Wastara alipotafutwa kuzungumzia madai hayo alisema ni kweli ana wakati mgumu na ameona ni vyema auze kile kinachowezekana ili aende akamalize matibabu ya mguu unaomsumbua.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364