-->

Watoto wa JK, Juma Nkamia Washinda Medali za Dhahabu Marekani

Dar es Salaam. Mtoto wa Rais mstaafu, Rashid Kikwete na mtoto wa mbunge wa Kondoa, Abdulrazak Nkamia wamelipa sifa Taifa baada ya kushinda medali za dhahabu katika mashindano ya Genius Olympiad, Marekani.

Genius Olympiad ni shindano la kimataifa la mazingira linalofanyika kila mwaka katika Chuo Kikuu cha Oswego kilichopo nchini Marekani.

Rashid ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuwa wamejifunza mambo mengi wakati wakiwa katika mashindano hayo na kuwataka wanafunzi wenzake kuacha kukata tamaa katika masomo.

Naye, Abdulrazak, ambaye ni mtoto wa mbunge wa Kondoa, Juma Nkamia amesema ushindi wao haukuwa rahisi kwa sababu kulikuwa na wanafunzi zaidi ya 1,200 kutoka nchi 73 duniani kote, ambao walishiriki mashindano hayo.

Katika mashindano hayo, Rashid na Abdulrazak walishinda medali ya dhahabu katika kipengele cha sanaa ya jamii huku Abdulah Rubaiya akishinda medali ya dhahabu katika kipengele cha filamu.

Awali, mkuu wa shule ya kimataifa ya Feza, Ali Yavuz, ambako washindi hao wanasoma, alisema kati ya wanafunzi 22 wa kitanzania walioshiriki mashindano hayo, wanafunzi watatu wamerudi na medali tatu za dhahabu na hivyo kuitangaza nchi kimataifa.

“Jumla ya wanafunzi 1,200 kutoka mataifa 73 duniani walishiriki katika mashindano ya Genus Olympiad yaliyofanyika juzi nchini Marekani, ambapo mashindano hayo yalihusisha vipengele vya utunzaji wa mazingira, utalii na utamaduni, ”amesema Yavuz.

Mbunge wa Viti Maalumu, Salma ambaye ni mke wa Rais mtaafu Jakaya Kikwete alikwenda kuwapokea wanafunzi hao jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

“Ni fahari kubwa kuona vijana wetu wamefanya juhudi katika mashindano haya, lakini pia naipongeza shule yao ya Feza kwa kuwatengeneza wanafunzi hawa hatimaye kuonekana vizuri katika uso wa dunia,” amesema Mama Salma ambaye ni mama mzazi wa Rashid.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364