-->

Wema Adai Kuwa Kajala ni Mtu Mzima Fulani Lakini Hana Hiki

WEMA6521

Wema Sepetu amesema hataki tena kuwa karibu na rafiki yake wa zamani Kajala Masanja kwa madai alishindwa kumtafuta na kumuomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya.

 

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV, Wema alisema Kajala kwa sasa anamchukulia kama mtu asiyemfahamu.

“Mimi mtu ambaye sitaki kujiassociate naye namtoa kabisa ndio maana naweza nikakaa nikakuuliza Kajala ni nani? Huu sio muda wa kumzungumzia na kumpa airtime,” alisema Wema.

 

“Kwa sababu nilishasemaga hata kwenye kipindi changu na nilimwambia natuja kumsaidia.”

Pia Wema amesema Kajala hajawahi muomba msamaha yeye mwenyewe tofauti na ile post ya Instagram aliyoomba radhi. Wema anadai alimshamunfollow na kumblock Kajala kwenye Instagram.

“Mimi sina kinyongo na mtu, unajua mtu ambaye ana kinyongo na mtu ni mtu ambaye hawezi kukaa bila kumuongelea mtu fulani. Mimi sijawahi kukaa na kumuongelea Kajala na nimemchukulia kama ni mtu ambaye ameshapita kama upepo. Hajui kutumia utu uzima wake ni mtu mzima for nothing, ni mtu mzima fulani lakini hana akili. Sio tu hana akili pia naona pia washauri wake ni wabaya,” alisisitiza Wema.

Pia Wema alifafanua kiini cha ugomvi wao na ni nani alisababisha yote kutokea.

“Kajala mimi ndiye aliyenizingua Mungu anajua kila kitu. Lakini mimi sikwenda kwenye Instagram kupost na kuandika Kajala kanizingua, mimi nilimfuata Kajala personal kwenye meseji nikamfuata nikamwambia nilichoweza kumuambia na hakukiona kwenye Instagram hata kumwambia najuta kumsadia nilimwambia kwenye kipindi lakini nilianza kumwambia kwenye meseji.”

Miaka miwili iliyopita, Wema alimlipia Kajala shilingi milioni 13 ili asifungwe jela kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili.

Mwaka 2015 wawili hao waliokuwa marafiki wakubwa waligombana kwa madai Kajala alitoka kimapenzi na mpenzi wa rafiki yake, Wema.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364