Zari: Sina Haja ya Kupima DNA,Tiffah ni Mtoto wa Diamond
Kwa wiki kadhaa kwenye kwenye mtandao wa Instagram kumekuwa na majibishano ya vijembe kati na Wema Sepetu na Zari hasa kuhusiana na uhalali wa mtoto wa Tiffah kama ni wa Diamond. Zari amepiga stori na @cloudsfmtz moja kwa moja kutoka Sauz.
‘’Ngoja nikwambie kitu mimi ni mzazi ni muda mrefu Wema na timu yake wamekuwa wakimsema mtoto wangu…Mara Oooh Tiffah Katunzi…Tiffah Ivan..Sasa ninachoshangaa Wema hayupo na Diamond sasa mambo ya Tiffah yanamuhusu nini? Haya hata kama mtoto ni mtoto wa hao watu wanaowataja yeye na ‘team’ yake inawahusu nini?,’’Zari.
‘’Yeye sio familia ya Diamond amebaki kuwa ‘ex’ kama akina Jokate,Wolper wote wametulia wanafanya mambo yao,kwanini Wema anatuma watu wamatukane mtoto wangu kuwa angekuwa mzuri tungehama mjini,mara mtoto mwenyewe mbaya,Zombi nimewavumilia sana ndio maana nikawajibu,’’Zari.
‘’Mbona wao wanafake maisha yao kuanzia magari,nyumba ,atafute kazi afanye au a’promote’ lipstick zake ..’No need for DNA Tiffah ni wa Diamond …Nimefunga mjadala,’’Zari.
Cloudsfm.com