-->

Wema na Idris Kama Chris Brown na Karrueche

Hii sasa kali, uhusiano wa mlimbwende kwenye tsnia ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ na Mchekeshaji, Idris Sultan umekuwa kama ule wa rapa, Chris Brown na aliyekuwa mpenzi wake Karrueche Tran, wazungu wanauiita ‘off and on.’

WEMA33

Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu.

Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana kutumia app ya Facetime, aliandika: That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu… ?

Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita.

Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika.

Mashabiki wa Wema walikasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram. Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:

Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?

Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja.

“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa.

Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364